Dk. Hamisi Kigwangalla Kutangaza Rasmi Nia ya Kuwania Ubunge wa Jimbo la Nzega 2010

Tuesday, March 2, 2010
Mwanasiasa machachari na chipukizi, Dk. Hamisi A. Kigwangalla, ambaye ni mkazi na mzaliwa wa wilayani Nzega, Tabora anajipanga kutangaza rasmi nia yake ya kuwania ubunge wa jimbo la Nzega kupitia chama cha mapinduzi. 

Dk. Kigwangalla, ambaye anajiweka kama ni mtu mwenye kupenda maendeleo, anayeona mbali na mwenye nia ya dhati ya kuwaendeleza wanaNzega na watanzania wenzake walio maskini zaidi, alikuwa na haya ya kusema: "...mungu akinijaalia ninapanga kutangaza rasmi nia yangu ya kuwania ubunge wa jimbo la Nzega kupitia CCM kwenye uchaguzi ujao (yaani wa Mwaka 2010), hili linakuja sana baada ya kufuatwa na kuombwa na watu mbalimbali wa rika tofauti tofauti....nimejifikiria sana na ninadhani kama kila kitu kitaenda sawa naweza kufuata ushauri wa watu, kwa sasa hivi bado nashauriana na familia yangu, ndugu, jamaa na marafiki, wakiona nisonge mbele basi ninapanga kutangaza hadharani kupitia vyombo vya habari mnamo wiki ya kuanzia Machi 08, 2010."

Dk. Kigwangalla ni mwanaharakati, mkulima na mjasiriamali kijana aliyezaliwa wilayani Nzega miaka takriban 35 iliyopita na ni msomi wa digrii tatu ikiwemo ya kwanza ya udaktari wa tiba za binadamu (Doctor of Medicine), ya afya ya jamii (MPH) na ya utawala wa biashara (MBA). Kwa sasa anajishughulisha na kilimo na mambo ya harakati za kuleta maendeleo kwa kinamama, watoto na makundi mengine yaliyo katika hatari zaidi.

11 comments:

ringomoses said...

Kidumu Chama Cha Mapinduzi!
Nimefurahishwa na uamuzi wako wa kuthubutu kwa mara nyingine kuomba nafasi ya kuwatumikia wananchi wa Nzega.
Kwa miaka michache ambayo nimekufahamu nina imani kuwa wana Nzega hawatafanya kosa wala kujutia kuwa na kiongozi wa aina yako.
Mwenyezi Mungu akutie nguvu katika mchakato wote wa kutafuta nafasi hiyo adhimu.
Nakutakia kila la Kheri!
Kada mwenzio,
Dkt. Moses Ringo (Muheza, Tanga)

Masangu Matondo Nzuzullima (MMN) said...

Dr. Hamisi. Hongera sana kwa uamuzi huu. Mabadiliko ya kweli yanahitajika katika jamii yetu na viongozi vijana kama nyinyi ndiyo chachu hasa ya maendeleo hayo.

Nakutakia kila la heri katika harakati zako hizi!

hamisi.kigwangalla said...

Daktari Moses Ringo, Kada wa Chama na Kiongozi mahiri wa umoja wa vijana, naomba nikushukuru sana kwa misifa tele uliyonimwagia na imani yako juu ya uwezo wangu. Ni imani yangu kuwa wakati ukijiri wanaCCM wenzangu wa Nzega hawatafanya makosa na wataniunga mkono. Niombee nifanikiwe ili niwatumikie kwa nguvu zaidi wajenga nchi wenzangu!

ringomoses said...

NTAZIDI KUKUOMBEA DUA INSHAAALAAH MWENYEZI MUNGU ATAKUJAALIA.
KILA LA KHERI KAKA!
Kidumu Chama Cha Mapinduzi!
Dkt. Moses Ringo (Muheza)

mumyhery said...

Mkuu kila la kheri, kaza buti!!!

hamisi.kigwangalla said...

ahsanteni sana wandugu zangu. Dua zenu ninazihitaji sana sasa na hata milele yote. Hii nia yangu ya kuamua kuingia kwenye kuwania Ubunge ni sawa na kutangaza nia ya kupigana vita!

Mungu atanifikisha salama, inshaallah.

Hamisi Kigwangalla.

hamisi.kigwangalla said...

Kaka Matondo bado uko US, na unafundisha? I can see it is a long time we haven't communicated

Masangu Matondo Nzuzullima (MMN) said...

Dr, ndiyo bado niko US nabangaiza. Tamaa ni kurudi nyumbani wakati mwafaka utakapofika. Tutawasiliana pembeni. Kila la heri!

Mwombeki Fabian, MD, MMCi said...

kaka kaza buti kumbuka "we are behind you but God before you"
all the best mkuu!!

Unknown said...

hongera kaka, nimekuona kwenye front page ya TAZAMA. Kaza buti unafanya vizuri sana. big up

hamisi.kigwangalla said...

Ahsante sana dada Lulu....naendelea kupigana tu! Kama kawaida yangu, we unanijua vizuri. Daima mbele. Wengi, haswa waliobahatika kufika jimboni Nzega, sasa hivi wananiambia kuwa niko sawa...sasa sijui hali itakuwaje tarehe 8/8 baada ya kura kuhesabiwa (maana it begins with hizi kura kabla ya vikao vya ndani ya chama!)

Ahsante sana kaka Mwombeki, pia nilipata na meseji yako. Nashukuru. Tuko pamoja.

Jamani mnikumbuke katika maombi yenu.

Post a Comment